MUHULA MPYA WA MASOMO | NOVEMBA 2021

Mkuu wa chuo cha mitambo (IHET) anapenda kuwatangazia kuwa masomo kwa muhula mpya mwezi Novemba, 2021 yataanza tarehe 8/11/2021 kwa waombaji wa fani za uendeshaji wa mitambo itumikayo kwenye ujenzi wa barabara, migodini na viwandani.

Kwa waombaji wa Dodoma, na MWANZA maombi  yanapokelewa chuoni IHET Nala Dodoma  na IHET Ilemela Mwanza . Kwa waombaji wa Dar es Salaam, maombi yanapokelewa chuoni IHET Kijitonyama kwa fani zote za ufundi wa mitambo, uendeshaji wa mitambo, udereva wa magari na kompyuta. Kwa mawasiliano zaidi tupigie simu namba 0754300200 au 0748221919 au 0719348778 au 0747175175.

Mafunzo ya ufundi kwa muda mfupi yanatolewa chuoni IHET Kijitonyama na Dodoma.