Muhula mpya wa masomo mwezi januari 2019

Mkuu wa chuo cha mitambo (IHET) anapenda kuwatangazia kuwa muhula mpya wa masomo utaanza tarehe 14/1/2019, wote mliochukua fomu za kujiunga mnakumbushwa kurudisha mapema kabla ya tarehe 7/1/2018. Mafunzo na kozi zitakazo tolewa ni pamoja na mafunzo ya uchomeleaji (welding), umeme wa magari (Auto electric), ufundi wa magari (mechanics), mafunzo ya uendeshaji wa mitambo na computa.

Fomu za kujiunga zinapatikana chuoni Kijitonyama na kwenye website ya chuo. Wote mnakaribishwa.