Mkuu wa chuo cha Mitambo na Tekinolojia (IHET) Dar es Salaam, anapenda kutangaza nafasi ya kazi FRONT OFFICE nafasi moja.
VIGEZO:
- Muombaji awe Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 30.
- Awe na sifa/elimu ya Cheti au Diploma kutoka chuo kinachotambulika.
- Awe na uwezo wa kusoma na kuandika vizuri kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili.
- Awe anajua kutumia Kompyuta; Programu kama MS. WORD, MS. EXCEL, EMAIL na Intaneti.
Waombaji wenye sifa watume CV na Barua ya Maombi kupitia email: recruitment@ihet.ac.tz
Maombi yatumwe kabla ya tarehe 20/8/2022