Mkuu wa chuo cha mitambo (IHET) anapenda kuwatangazia kuwa masomo kwa mwaka mpya wa masomo 2022, yataanza tarehe 17/1/2022 kwa waombaji wa fani za:-
- Ufundi wa mitambo
- Ufundi wa magari makubwa na madogo
- Uchomeleaji na
- Umeme wa magari.
Maombi ya kujiunga na masomo ya ufundi ya muda mrefu (Long Course 2022) yanapokelewa chuoni IHET Kijitonyama Dar es Salaam, IHET Nala Dodoma, na Ilemela MWANZA. Mwisho wa kupokea fomu ni tarehe 27/12/2021 hivyo wote waliochukua na kujaza fomu za maombi wanakumbushwa kurudisha fomu hizo mapema.
Kwa waombaji wa fani za uendeshaji wa mitambo (Plant Operator), udereva wa magari na kompyuta maombi yanapokelewa chuoni IHET Kijitonyama Dar es Salaam, IHET Nala Dodoma, na Ilemela MWANZA.
Fomu za kujiunga, fomu ya taratibu za kujiunga na nakala ya malipo vinapatikana kwenye tovuti ya chuo www.ihet.ac.tz
Kwa mawasiliano zaidi tupigie simu namba 0754300200 au 0748221919 au 0719348778 au 0747175175.