MUHULA MPYA WA MASOMO | NOVEMBA 2022

Mkuu wa chuo cha mitambo (IHET) anapenda kuwatangazia kuwa masomo kwa muhula mpya mwezi NOVEMBA, 2022 yataanza tarehe 7/11/2022 kwa waombaji wa fani za uendeshaji wa mitambo itumikayo kwenye ujenzi wa barabara, migodini na viwandani.

Mafunzo yanafanyika kwa kutumia mitambo ya kisasa ya kufundishia (Simulators) pamoja na mazoezi (practical) kwenye fani husika.

Waombaji wa kozi za muda mfupi za ICT masomo yataanza tarehe 7/11/2022.

Kwa waombaji wa Dodoma, na MWANZA maombi  yanapokelewa chuoni IHET Nala Dodoma  na IHET Mwanza, Barabara ya Nyerere mtaa wa Liberty karibu na benki ya NBC. Kwa waombaji wa Dar es Salaam, maombi yanapokelewa chuoni IHET Kijitonyama kwa fani zote za ufundi wa mitambo, uendeshaji wa mitambo, udereva wa magari na kompyuta. Kwa mawasiliano zaidi tupigie simu namba 0754300200 au 0748221919 au 0719348778 au 0687108773