Mkuu wa chuo cha mitambo (Institute of Heavy Equipment and Technology – IHET) kwa kushirikiana na chuo cha EKAMI cha nchini FINLAND anapenda kuwatangazia mafunzo ya muhula mpya wa masomo mwaka 2020, ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 9/3/2020 kwa utaratibu ufuatao;
- Ada ya mafunzo ni shilingi milioni mbili na laki mbili (2,200,000/=)
- Mwombaji atatakiwa kulipa kiasi kisichopungua shilingi laki tano ( 500,000/=) wakati wa kujiunga.
- Mwisho wa malipo ya ada iliyobakia yanatakiwa kulipwa kabla ya tarehe 1/6/2020.
- Mwanafunzi hatopelekwa kwenye mafunzo kwa vitendo (field training) na kupewa cheti mpaka akamilishe kiasi cha ada kilichobaki.
- Mafunzo kwa vitendo yanatarajiwa kuanza mapema mwezi wa tano.
Wote mnakaribishwa
Imetolewa na idara ya masoko, IHET